Thursday 9 May 2013

NEWS

Benki ya dunia yasema Kenya itashindwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia-by CRI

(GMT+08:00) 2013-05-09 11:12:23
Benki ya dunia jana ilisema Kenya haiko kwenye njia sahihi ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia kabla ya mwaka 2015 kutokana na kuwa umaskini wa kupindukia haujapunguzwa licha ya juhudi zilizofanywa. Mchumi mwandamizi wa Benki ya dunia Bi Vandana Chandra amesema hali hiyo inatokana na kuwa sera zilizowekwa na Kenya bado hazijatekelezwa vizuri. Hata hivyo amesema hii haina maana kuwa hakuna matumaini, kwa kuwa kama juhudi zikiongezwa mafanikio yanaweza kupatikana.
Ripoti ya pamoja iliyotolewa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF inaonesha kuwa malengo ya kuleta usawa wa kijinsia na kupunguza vifo vya watoto hayataweza kufikiwa kabla ya mwaka 2020. Bi Chandra amesema bado watu wengi hawana kazi zinazolipa mishahara mikubwa, ili kuwawezesha watu waishi na zaidi ya dola 1.25 kwa siku. Ameishauri serikali kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta binafsi hasa kwenye sekta za uzalishaji na huduma.

No comments:

Post a Comment